NA LAYLAT KHALFAN

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imesema kuchelewa kwa ujenzi wa kiwanja Wilaya ya Magharibi A,  kunatokana na eneo hilo kuwa na mgogoro, kwani katika eneo hilo kuna njia inayoelekea kwa muwekezaji wa utalii.

Waziri Lela Muhamed Mussa alitoa kauli hiyo wakati akijibu suala  aliloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Mfenesini Machano Othman Said, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, ambapo mwakilishi huyo alitaka kujua ni sababu gani za msingi zinazosababisha ujenzi huo kuchelewa kuanza.

Alisema kutokana na hali hiyo uongozi wa Wilaya ulionesha wasiwasi juu ya mgogoro huo na kuamua kusitisha ujenzi huo.

Alisema pia katika eneo hilo hakukua na mkataba uliotiwa saini kati ya wizara na mkandarasi aliyetarajiwa kujenga kiwanja hicho.

“Gharama za ujenzi za mkandarasi ni za chini sana ikilinganisha na makadirio ya Wakala wa Ujenzi, hali ambayo ina kila sababu ya kuamini kuwa mkandarasi asingemaliza kazi kwa kiwango kinachotakiwa”, alisema waziri huyo.

Akizungumzia pesa za ujenzi huo, alisema kiwango cha fedha kinachotarajiwa kutumiwa katika ujenzi wa kiwanja hicho kwa awamu ya kwanza  ni shilingi millioni 400,000,000.

Aidha, alisema viwanja vya wilaya hiyo vilivyojengwa vilisainiwa na Wakala wa Majenzi na ripoti ya kitaalam imeonesha kuwa, viwanja vimekidhi mahitaji ya mkatab