NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kushuka Dimbani leo Juni 13 kuvaana na timu ya taifa ya Malawi, kwenye mchezo wa kirafiki uliopo kwenye Kalenda ya FIFA.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars waliingia kambini Juni 4 katika Hotel ya Tiffany iliyopo hapohapo jijini chini ya kocha Kim Paulsen.

Timu hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi yake kwenye viwanja viwili vya JKM Park na Benjamini Mkapa kwa nyakati tofauti tofauti.

Viingilio vilivyotaja na TFF vya mchezo huo VIP B&C-ni Shilingi 5000 huku mzunguko ukiwa ni Shilingi 2000.

Huku wakiwaomba mashabiki kuhudhuria kwenye mchezo huo naiunga mkono timu yao ili ifanye vizuri.