NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Soka la Tanzania ( TFF) kupitia katibu wake Kidao Wilfred, limetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko juu ya suala zima la uchukuaji wa fomu.

Wagombe wa kiti cha urais waliokwenda TFF kuchukua Fomu ya kugombea nafasi hiyo, walikuwa wakilalamikia kukosa udhamini wa vyama vya mikoa kutokana na idadi kubwa iliyowekwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika mkutano uliofanyika Shirikisho la Soka TFF , Kidao alisema kuhusu malalamiko hayo, wao sio walioweka lakini ni mabadiliko ambayo yalifanyika muda mrefu.

Alisema TFF wao hawampangii mwanachama nani wa kumdhamini, ila wanachama wenyewe ndio wataamua nani watampa, lakini ni utaratibu ambao haukuanza jana  na hawakuubadilisha wao kwa mapenzi binafsi.

“ Hakuna chochote ambacho TFF imebadilisha kwa maslahi binafsi, hayo mabadiliko yamefanyika tangu 2004 na mengine yalibadilika 2019 .

Kidao aliendelea  kusisitiza  kuwa ni vyema kamati ya uchaguzi ikaachiwa majukumu yao, kwani wao ndio ambao wanafahamu, nani amekosa kwani hata yeye katibu hawezi kufahamu mpaka muda muafaka utakapofika.