NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

BAADA ya Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Vodacom kutangaza kutoendelea kudhamini ligi kwa msimu ujao, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Almasi Kasongo amewatoa hofu wapenzi wa soka.

Vodacom walitoa maamuzi hayo wakidai kwamba walipata hasara.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana, Kasongo alisema kampuni hiyo ilishindwa kutimiza makubaliano ambayo walikubaliana kwenye mkataba shilingi Bilioni 3 kwa msimu.

Alisema kampuni hiyo ilikuja na mapendekezo ya kwenda kulipa shilingi Millioni 500 huku wakiahidi kulipa kiasi tena kiasi kilichobaki msimu wa 2022/2023

“Kwa pamoja tulikubaliana  kuwa badala ya kulipa Milioni  500 walipe Milioni 600 na klabu zilikubali mapendekezo hayo,”alisema