Jules Kounde
MANCHESTER United wanakabiliwa na ushindani katika kumnasa mlinzi wa Sevilla, Jules Kounde huku Barcelona pia ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Mundo Deportivo).
Carlo Ancelotti
KOCHA, Carlo Ancelotti ameondoka Everton ili kuifundisha Real Madrid kwa mara ya pili. Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 61 ambaye aliongoza Real kwa miaka miwili kati ya 2013 na 2015 ameondoka Goodison Park baada ya miezi 18 ili kuiziba nafasi iliyoachwa wazi na Zinedine Zidane.(Athletic).
Lionel Messi
MSHAMBULIAJI wa Argentina, Lionel Messi (33), yuko karibu kukubali mkataba wa miaka miwili kubakia Barcelona. (AS).
Raheem Sterling
ARSENAL wanaongoza kwenye mbio za kumpata winga wa Manchester City, Muingereza Raheem Sterling (26), mpango ambao unaweza kumzuia mshambuliaji, Harry Kane (27), kujiunga na ManCity akitokea Tottenham. (Sun).
Andre Onana
KLABU ya Arsenal wanajiandaa kukamilisha taratibu za kumsajili mlinda mlango wa Cameroun, Andre Onana (25), kutoka Ajax kwa pauni milioni 1.7 (Nos-in Dutch).
Romelu Lukaku
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich binafsi ana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Ubelgiji anayekipiga Inter Milan, Romelu Lukaku (28) na kumrejesha Stamford Bridge. (Eurosport).
Thomas Tuchel
KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel atapatiwa mpaka pauni milioni 200 kwa ajili ya matumizi ya msimu huu wa kiangazi. (Metro).
Miralem Pjanic
KIUNGO wa Barcelona, Miralem Pjanic (31), anataka kurejea Juventus. (Tuttosport).
Gianluigi Donnarumma
KOCHA mpya wa Roma, Jose Mourinho, anatazamia kumsajili mlinda mlango wa AC Milan, Muitaliano Gianluigi Donnarumma (22). (Mirror).
Boubakary Soumare
MPANGO wa Leicester City kwa ajili ya kiungo wa kati wa Lille, Boubakary Soumare (22), unaweza kukamilika haraka kuliko ilivyodhaniwa baada ya klabu hiyo kuondolewa katika michuano ya Euro. (Leicester Mercury).
Pedro Goncalves
MANCHESTER United wanamtolea macho kiungo wa Sporting Lisbon, Pedro Goncalves (22). (Record).
Romain Perraud
KLABU ya Leeds United itatafuta mbadala baada ya kushindwa bei ya kumpata beki wa kushoto wa Ufaransa, Romain Perraud (23). (Football Insider).