Hector Bellerin
KLABU ya Juventus wanamtaka, Hector Bellerin na huenda wakamuachia tena kiungo wa Wales, Aaron Ramsey (30), katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na washika bunduki.(Sport).

Nuno Espirito Santo
KOCHA wa zamani wa Wolves, Nuno Espirito Santo anakaribia kuteuliwa kuwa meneja wa Crystal Palace. (Telegraph).

Lorenzo Pellegrini
LIVERPOOL wametangaza dau la pauni milioni 25.8 kumnunua nahodha wa Roma na kiungo wa Italia, Lorenzo Pellegrini (24), kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30). (Corriere dello Sport).

Saul Niguez
KLABU ya Atletico Madrid wamemtoa kiungo wa Hispania, Saul Niguez (26), kwa Manchester City ili wampate mshambuliaji wa Ureno, Bernardo Silva (26). (Times).

Erling Braut Haaland
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland (20), anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge. (Telegraph).

Takumi Minamino
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na Japan, Takumi Minamino, anahusishwa na kurejea Southampton ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita baada ya kocha, Ralph Hasenhuttl, kuulizia mpango wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26. (HampshireLive).

Dani Ceballos
MUHISPANIA, Dani Ceballos (24), amesema, anataka kurejea La Liga msimu ujao baada ya mkataba wake wa mkopo Arsenal kutoka Real Madrid kumalizika. (Cadena SER).