Achraf Hakimi
KLABU ya Chelsea inataka kumsajili beki wa kulia wa Inter Milan na Morocco, Achraf Hakimi (22) ambaye amekuwa akinyatiwa na Paris St-Germain. (Times).
Rafael Benitez
KOCHA wa zamani wa Liverpool na Newcastle, Rafael Benitez anagombea nafasi ya umeja iliyoachwa wazi Everton. (Mail).
Elseid Hysaj
KLABU ya Napoli inapanga kuwaaga wachezaji wao kadhaa muhimu msimu huu wa joto.
Kalidou Koulibaly na Fabian Ruiz huenda wakauzwa, Elseid Hysaj na Nikola Maksimovic wataondoka kwa uhamisho wa bure na Tiemoue Bakayoko atarudi Chelsea baada ya mkopo wake.(Gazzetta dello Sport).
David Moyes
Meneja wa West Ham David Moyes anakaribia kukubali kandarasi mpya ya miaka mitatu.
Kocha huyo wa zamani wa Everton na Manchester United anatarajiwa kuzawadiwa kwa msimu ambao utawashuhudia wagonga ‘nyundo’ wakiwa katika nafasi bora mwisho wa kampeni.(Telegraph).
Jeremie Boga
KLABU ya Lyon itatoa kipaumbele uhamisho wa kiungo wa Sassuolo, Jeremie Boga, msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amefanikiwa katika ‘Serie A’ na Sassuolo inaweza kuwa na hamu ya kurudisha ada ya uhamisho kwa Boga anapoingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake.(Le10Sport).
Ryan Bertrand
KLABU ya Leicester City imejiunga na mbio za beki wa pembeni wa Southampton, Ryan Bertrand.