FLORIAN NEUHAUS
LIVERPOOL inafanya mazungumzo na Borussia Monchengladbach ili kumsajili kiungo wa Ujerumani Florian Neuhaus, 24. (Sport1 – in German)
PAULO FONSECA
MENEJA wa zamani wa Roma Paulo Fonseca amekubali kimsingi mkataba wa miaka miwili kuinoa Tottenham. (Telegraph)
BEN WHITE
ARSENAL wanaandaa mpango wa kumsajili beki wa kati wa Brighton na England Ben White, 23. (Athletic)
MANUEL LOCATELLI
GUNNERS pia wanamtazama kiungo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 23 Manuel Locatelli. (Sky Sport Italia, via Metro)
Jadon Sancho
WINGA wa Uingereza Jadon Sancho, 21, atakuwa mshindi wa pili kwa juu Manchester United, nyuma ya kipa David de Gea, ikiwa atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto. (Mail)
SERGIO RAMOS
SEVILLA wamempa mlinzi wa kati wa Uhispania Sergio Ramos, 35, mkataba wa miaka mitano. Ramos amemaliza mkataba na Real Madrid msimu huu wa joto. (esRadio – in Spanish)
SAUL NIGUEZ
CHELSEA inavutiwa na kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez, 26, lakini Manchester United na Juventus wanabaki kuwa vipenzi vya kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania. (Mundo Deportivo – in Spanish)
ROBERT LEWANDOWSKI
MSHAMBULIAJI wa Poland Robert Lewandowski, 32, yuko tayari kuondoka Bayern Munich. (AS – in Spanish)
NIKOLA VLASIC
EVERTON wanafikiria kumsajili tena mshambuliaji wa Croatia Nikola Vlasic, 23, kutoka CSKA Moscow – miaka miwili baada ya kumuuza. (Star)
SERGE AURIER
BEKI wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 28, amekubaliana masharti ya kibinafsi na Paris St-Germain. (Football Insider)
DANNY ROSE
MLINZI wa pembeni wa England Danny Rose, 30, anakaribia kujiunga na Watford baada ya kuondoka Tottenham. (Watford Observer)
GIANLUIGI DONNARUMMA
MLINDA mlango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 22, anakaribia kukamilisha uhamisho wa bure kwenda Paris St-Germain. Ataondoka AC Milan msimu huu wa joto wakati mkataba wake utamalizika. (Calciomercato – in Italian)