Bernardo Silva
KIUNGO wa Manchester City, Bernardo Silva (26), angependelea kutimka msimu huu, lakini, Meneja Pep Guardiola amegoma kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.
(Athletic).
Raheem Starling
WINGA wa England na Manchester City, Raheem Sterling (26), anatarajiwa kusalia Etihad msimu ujao, licha ya kuhusishwa kwake kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu England. (Manchester Evening News).
Cristiano Ronaldo
MANCHESTER United imepeleka dau la pauni milioni 17 ambalo litakuwa la mwaka mmoja kwa ajili ya kumrejesha mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo kutoka Juventus, katika mpango ambao utashuhudia kiungo Mfaransa, Paul Pogba (28), akienda upande wa pili. Hata hivyo, chaguo la Ronaldo ni Paris St-Germain. (Gazzetta dello Sport).
Hector Bellerin
KLABU ya Juventus wanamtaka, Hector Bellerin na huenda wakamuachia tena kiungo wa Wales, Aaron Ramsey (30), katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na washika bunduki.(Sport).
Nuno Espirito Santo
KOCHA wa zamani wa Wolves, Nuno Espirito Santo anakaribia kuteuliwa kuwa meneja wa Crystal Palace. (Telegraph).
Lorenzo Pellegrini
LIVERPOOL wametangaza dau la pauni milioni 25.8 kumnunua nahodha wa Roma na kiungo wa Italia, Lorenzo Pellegrini (24), kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum (30). (Corriere dello Sport).