Conor Coady
KLABU ya Everton inataka kumsaini nyota wa Wolves na England, Conor Coady (28).(Football Insider).

Erling Braut Haaland
KLABU ya Chelsea inataka kujenga uhusiano mzuri na Borussia Dortmund kwani wanatarajia kusaini wachezaji wao wawili bora zaidi, mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland (20), na kiungo wa kati wa Uingereza, Budaham (17).(Star).

Raphael Varane
MANCHESTER United wamepata ombi la kufungua ofa ya pauni milioni 50 kwa beki wa Real Madrid na Ufaransa, Raphael Varane, lakini, Real wanataka pauni milioni 80 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.(Manchester Evening News)

Sergio Ramos
KUONDOKA kwa Sergio Ramos kutoka Real Madrid kunaweza kudhoofisha mipango ya United ya kumsajili Varane baada ya wababe hao wa Hispania kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na beki huyo wa kati. (Times).

Nat Phillips
KLABU ya Newcastle United imemuongeza mlinzi wa Liverpool, Nat Phillips katika orodha ya wachezaji inaowafukuzia, lakini, itawalazimu kupambana na Burnley kumnasa beki huyo wa kushoto raia wa Uingereza, ambaye hatarajii kupata nafasi atakapopona majeruhi Virgil Van Djik, Joe Gomez na Joel Matip. (Mail).

Jack Grealish
CHELSEA wanapewa nafasi kubwa ya kumnasa kiungo wa England na Aston Villa, Jack Grealish msimu huu, wakitarajiwa kuzipiku klabu za jiji la Manchester, kwenye mbio za kupata saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes).

Kieran Tierney
MLINZI wa kushoto wa Arsenal na Scotland, Kieran Tierney (24), anahusishwa na uhamisho wa kuhamia Manchester City. Kocha wa zamani wa Celtic, Neil Lennon, ndiye anayemuhusisha nyota huyo na uhamisho huo. (Times).

Boubakary Soumare
KLABU ya Leicester City inatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo Mfaransa, Boubakary Soumare wiki hii. Klabu za Wolves na Everton nazo zinavutiwa na kinda huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye kwa sasa anachezea mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa. (Mail).

James Tarkowski
MLINZI wa Burnley, James Tarkowski anatarajiwa kutua West Ham msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa England, mwenye umri wa miaka 28 amecheza michezo 36 msimu uliopita wakati Burnley ikinusurika tena kushuka daraja. (Football Insider).

Matheus Nunes
KLABU ya Everton inamuwania nyota wa Sporting Lisbon, Matheus Nunes (22). Dau la kuanzia la pauni milioni 15 limetengwa kwa ajili ya kiungo huyo raia wa Brazil, linaweza kufikia mpaka pauni milioni 17 ukijumlisha na masharti mengine. (Record).

Achraf Hakimi
KLABU ya Chelsea inataka kumsajili beki wa kulia wa Inter Milan na Morocco, Achraf Hakimi (22) ambaye amekuwa akinyatiwa na Paris St-Germain. (Times).

Elseid Hysaj
KLABU ya Napoli inapanga kuwaaga wachezaji wao kadhaa muhimu msimu huu wa joto.
Kalidou Koulibaly na Fabian Ruiz huenda wakauzwa, Elseid Hysaj na Nikola Maksimovic wataondoka kwa uhamisho wa bure na Tiemoue Bakayoko atarudi Chelsea baada ya mkopo wake.(Gazzetta dello Sport).

Jeremie Boga
KLABU ya Lyon itatoa kipaumbele uhamisho wa kiungo wa Sassuolo, Jeremie Boga, msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amefanikiwa katika ‘Serie A’ na Sassuolo inaweza kuwa na hamu ya kurudisha ada ya uhamisho kwa Boga anapoingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake.(Le10Sport).

Ryan Bertrand
KLABU ya Leicester City imejiunga na mbio za beki wa pembeni wa Southampton, Ryan Bertrand.
Bertrand hivi karibuni alitangaza kuwa ataachana na ‘Watakatifu’ kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto na mlinzi huyo hatakuwa ufupi juu ya chaguzi kwa klabu yake ijayo. (talkSPORT).

Randal Kolo Muani
KLABU ya Lyon wana mchezaji wa Nantes, Randal Kolo Muani katika macho yao kufuatia msimu mzuri.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa mzuri katika kipindi hichi, na amevutia macho ya klabu nyengine Ulaya, ikiwemo Eintracht Frankfurt.(Le10Sport).

Adam Reach
KLABU ya Norwich City inaweza kuimarisha usajili wao wa Ligi Kuu ya England kwa nyota wa Sheffield Wednesday, Adam Reach.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakuwa nje ya mkataba na Bundi hao na anatarajiwa kuondoka bure. (Football Insider).