KAMPALA, Uganda
KOCHA Mkuu wa Uganda, Morley Byekwaso ametaja kikosi cha wachezaji 40 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji iliyopangwa kufanyika nchini Ethiopia.
Michuano hiyo ni ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23, lakini, sheria za mashindano zinaruhusu wachezaji watatu wa zaidi ya umri kwa timu yoyote.

Uganda itatumia fursa ya sheria hii na kutaja wachezaji watatu wakubwa kwa ajili ya uzoefu na muongozo kwa vijana. Wachezaji wakubwa waliotajwa ni walinda milango, Watenga Ismail (Chippa United FC) na Charles Lukwago (KCCA FC), mshambuliaji Yunus Ssentamu (Vipers SC), beki Murushid Juuko (Express FC) na kiungo, Said Kyeyune (hawajafungamana).

Ni orodha hii ambayo wachezaji watatu watatajwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa mashindano hayo.
Kikosi kamili kinaundwa na walinda milango, Watenga Ismail (Chippa United FC), Lukwago Charles (KCCA FC), Otim Dennis (Express FC), Keni Saidi (SC Villa), Kibowa Eric (UPDF FC), Matovu Hassan Muyomba (KCCA FC).

Walinzi ni ni Kizito Mugweri Gavin (SC Villa), Begisa James Penz (UPDF FC), Walusimbi Enock (Express FC), Kayondo Abdu Aziizi (Vipers SC), Ndahiro Derrick (SC Villa), Kaddu George (Wakiso Giants FC), Juuko Murushid (Express FC), Musa Ramathan (KCCA FC), Ssemakula Kenneth (BUL FC), Magambo Peter (KCCA FC) na Mukundane Hillary (Mbarara City FC).

Viungo ni Byaruhanga Bobosi (Vipers SC), Kiggundu Derrick (Soltilo Bright Stars FC), Watambala Abdul Karim (Vipers SC), Kyeyune Saidi (Unattached), Sserwadda Steven (KCCA FC), Ssenyonjo Hassan ( Wakiso Giants FC), Anukani Bright (KCCA FC), Mugulusi Isam (Busoga United FC), Kabonge Nicholas ( SC Villa) na Salim Abdallah (SC Villa).

Washambuliaji ni Bogere Ivan (Wakiso Giants FC), Masereka Saddam (SC Villa), Poloto Julius (KCCA FC), Basangwa Richard (Vipers SC), Yiga Nagib (Vipers SC), Kiwanuka Hakim (Proline FC), Ssentamu Yunus (Vipers SC), Kakooza Derrick (Police FC), Ssenyonjo Samuel (KCCA FC), Anaku Sadat (KCCA FC), Ssebufu Frank (Wakiso Giants FC), Kambale Eric Kenzo (Express FC) and Lwanga Charles (KCCA FC).
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Julai 3 hadi 18 nchini Ethiopia.(Goal).