Ni imani potofu yenye kuutukuza uyahudi

KATIKA siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kuwapigia simu watu wengine wasiowafahamu wakiwaeleza kuwa nao wanataka kujiunga na chama.

Kwa bahati mbaya anayepigiwa simu, hugubikwa na masuala kadhaa, ambapo la kwanza miongoni mwa masuala hayo, huuliza chama gani hicho? Jawabu linalotoka kwa aliyepiga simu ni kwamba nataka kuwa mwanachama wa ‘freemason’.

Kupokea simu za namna limekuwa jambo la kwaida sana hasa za watu kutoka upande wapili wa Jamhuri ya muungano, huku anayepiga simu hizo akiomba astiriwe pindipo atakapofanikiwa kuwa mwanachama.

Wanaopiga simu za namna hii ni vijana ambao huvutiwa sana na yale wanayoyasikia kwamba wanachama wengi sana wa ‘freemason’, wamekuwa matajiri wana fedha za kutupa.

Bila shaka vijana huvutiwa na umasonia ili wawe matajiri, ila sidhani kama wanaelewa kwa undani chanzo cha dhana hii potofu na malengo yake.

CHANZO CHA UMASONIA

Umasoni ni chama cha siri kabisa cha kiyahudi na kilianzishwa katika enzi za kiroma sehemu za Aurshalim katika mji wa Jerusalem wakati wa ufalme wa Herodus Aghriba.

Dhana hii ilianzishwa na utawala wa mfalme huyo kwa ajili ya kuua watoto katika mji wa Bethlehem kwa hofu ya kuzaliwa Nabii Issa (Yesu), ambaye kwa mujibu wa imani yake, ni kwamba ujio wa Yesu ndio mwisho wa utawala wote wa Herodus.

Umasoni ulitambulika kwa utata na mtindo wake ulio na amri madhubuti. Malengo makuu yalikuwa ni kuhakikisha mamlaka yanabaki kwa mayahudi duniani kote.

Kwa kawaida imani hii potofu inahubiri upagani, utenganifu wa jamii na upotofu. Jumuiya hii inachagua wajumbe wake miongoni mwa watu maarufu kwenye nyanja ambazo zina nafasi kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Kitabu cha ‘simplified encyclopaedia’, kimeandika na kuchapisha kutoka WAMY (Baraza La Vijana Waislamu Duniani – World Assembly of Muslim Youth – Saudi Arabia) kinafafanua kwamba muasisi wa jumuiya hii ni Herdous Aghriba mfalme wa kiroma kwa msaada wa wasaidizi wa kiyahudi.

Hivyo, mwanzo wake ulitokana na ujanja, hila na mageuzi. Inachagua zana za utambulisho, majina na alama ili kueneza hofu na kuwafanya watu kuamini katika habari zisizo sahihi.

Katika maandishi yake Rabai Laquiz anasema kuwa umasoni unatokana na mayahudi kwa mujibu wa historia yake, uongozi wake, mafundisho yake, zana zake za siri na kazi zake za ubunifu.

Laquiz anasema kuwa mikakati ya mayahudi kuleta umasoni ulilenga kuwaadhibu wakristo, kuwaua viongozi, kuwakata vichwa, kuwapiga pande na kuizuia dini yao kuenea.

MAANA YA UMASONIA

Neno ‘mason’ lina maana ya yule mwenye kujenga nyumba. Hivyo ‘Free masons’ lina maana ya Wamasoni walio huru. Hii ndio ilikuwa haswa alama yao wakati walipokuwa wakifanya kazi zao (za kujenga nyumba).

Hata hivyo, jina hilo lipo mbali na tafsiri hiyo, enzi hizo ndio zilikuwa mwanzo wa umoja huu. Lakini vitu vilianzia pale Adam Webshawit, Mkiristo aliyeingia kwenye upagani, alipovutiwa na umoja huu ambao alidhani utamsaidia kuimiliki dunia yote.

Mara ya mwisho kutimu kazi hii ilikuwa ni mwaka 1776 M, na bodi ya mwanzo kuanzishwa ndani ya kipindi hicho (Bodi ya Torani), ilipewa jina baada ya huyo shetani wao waliokuwa wakimwabudia. Ukweli ni kwamba, Webshawit alikuwa ni mtu wa mwanzo aliyeanzisha mipango ile ile ya umasoni.

MADHUMUNI YA UMASONIA

Azma ya mwanzo ya umasoni ni kuupiga vita ukristo. Baadaye, azma zao ziliendelea kupiga vita dini zote, lengo likuwa nikuirudisha tena Israel na kuitoa Palestina.

Umasonia una malengo muhimu na imani zao kuu za wajumbe wa jumuiya hii ni, wanaitakidi kwamba imani kwa Allaah, Mitume na Vitabu kama ni upuuzi na hawaamini chochote katika ghayb.

Aidha wafuasi wa imani hiyo potofu, wanashiriki kwa hali zote kubadili serikali ili kuweka serikali ambayo inawakubali wao pamoja na mawazo yao.

Kwa kawaida wanaamini na kuhubiri ukombozi wa ngono na kumuona mwanamke kama ni aina fulani ya umiliki.

Wamasonia wanafanya bidii kuharibu mataifa mengine isipokuwa taifa la kiyahudi na kuanzisha migongano ya kudumu baina yao katika maaifa mengine.

Ni wafanya biashara ya silaha sehemu mbalimbali duniani ili kuendeleza migogoro na migongano huku pia wanafanya kila jitihada ya kuendeleza ukabila na uadui.

Msingi wa umasoni ni kuua na kuharibu kanuni za maadili kwa kutumia hongo kupitia ngono na pesa ili kuwavutia wenye kutoa maamuzi.

Wanafanya uchunguzi wa kudumu (na kuzifanyia kazi) ili kuwazuia waislamu na kuwapunguza kupitia aina zote (birth control).