NA MOHAMMED RASHID (DOMECO)

WADAU wa michezo nchini wamelitaka Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) na Serikali ya Mapinduzi, kutafuta wadhamini watakao dhamini ligi kuu ya Zanzibar na kusaidia kuleta ushindani kwa timu na wachezaji kushindana .

Wakizungumza na gazeti hili walisema ligi ya Zanzibar kwa sasa haina mvuto kama mashindano ya ndondo na kusababisha wachezaji wengi kujikita katika mashindano ya ndondo.

Aidha walisema timu nyingi zinajiendesha zenye na kutumia gharama kubwa katika uendeshaji, kama kutajitokea wadhamini basi gharama za uendeshaji wa timu nyingi zitapungua.

Walisema kunautofauti mkubwa wa shirikisho la soka la Zanzibar na shirikisho la Mpira la Tanzania katika suala la kutafuta wadhamani na uendeshaji wa ligi .

Aliongeza timu nyingi za Zanzibar kwa sasa hazifanikiwi katika mashindano ya klabu bingwa  Afrika kwa sababu ya kutokuwepo kwa wadhamini watakaotoa hamasa kwa wachezaji na timu zinazoshiriki mashinano hayo.