NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KUELEKEA uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), unaotarajiwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu mkoani Tanga, watu tisa wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbali mbali kwenye uchaguzi huo.

Wanafamilia hao walichukua fomu juzi katika ofisi za (TFF) zilizopo Ilala Jijini Dar es Salaam.

Ukiachilia mbali fomu kupatikana kwenye Shirikisho la Soka lakini pia zinapatika kwenye mtandao kupitia tovuti ya (TFF).

Waliochukua nafasi yakuwania nafasi ya Urais  Deogratius Mutungi, Evans G Mgeusa,Oscar Oscar, Zahor Mohammed Hajji, Wallace Karia.

Waliochukua fomu za ujumbe wa kamati ya utendaji ni  Lameck Nyambaya,Liston Katabazi na Michael Petro (Kanda) namba 1- Dar es Salaam,Lindi,Morogoro,Mtwara na

Pwani,Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 2 Arusha,Kilimanjaro Manyara na Tanga)

Mwisho wa kuchukua nakurudisha fomu ni Juni 12 mwaka huu.