NA VICTORIA GODFREY
WACHEZAJI wanne wa timu ya Taifa ya wanaume ya Mpira wa Wavu wanatarajia kushiriki Mashindano ya Kombe la Afrika yatakayoanza kutimua vumbi Juni 21 – 28 mwaka huu Agadir nchi Morocco.
Timu hiyo iliibuka vinara katika Mashindano ya awali ya Kanda ya tano kwa kushinda mechi zote na kupata nafasi ya kusonga hatua ya mbele ambayo yalifanyika Disemba 2019,Entebe nchini Uganda.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Meja Jenerali Mstaafu Patrick Mlowezi aliwataja wachezaji hao ni David Neeke, Ford Edward na Ezekiel Rabson na Joseph Mafuru watakuwa chini ya kocha Alfred Selengia ambaye ni mkufunzi wa makocha Ufukweni wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Barani Afirika (CAVB).
“Tunashukuru shindano la awali tulifabikiwa kufanya vyema na sasa tunakwenda awamu nyingine ,hivyo vikosi vyetu vitaanza rasmi mazoezi tayari wapo kambini,” alisema Mlowezi.
Mwenyekiti huyo alisema lengo ni kutafuta nafasi ya kushiriki michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka huu Tokyo nchini Japan.
Alisema TAVA inaomba wadau wa michezo, wafanyabiashara, Kampuni kujitokeza kuzisaidia timu kwa hali na mali ili timu iweze kujiandaa.