POURT LOUIS, MAURITIUS

WAZIRI mkuu wa zamani wa Mauritius, Anerood Jugnauth, ambaye aliongoza mabadiliko ya uchumi wa taifa hilo la kisiwa na kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi, amefariki akiwa na umri wa miaka 91.

Kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo alisema “Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Sir Anerood Jugnauth kilichotokea Juni 3 kutokana na ugonjwa,” Rais Prithvirajsing Roopun alitangaza Alhamisi jioni.

Taarifa zilisema kuwa mazishi yake yalifanyika Ijumaa sambamba na kutangaza siku mbili za maombolezo na bendera ya taifa imeshushwa hadi nusu mlingoti kwenye majengo yote ya umma.

Jugnauth aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza kati ya mihula sita mnamo mwaka 1982, ambapo pia atatumikia vipindi viwili na kuhudumu kwa miaka 35 ya kazi.

Alijiuzulu mnamo mwaka 2017 na akampa hatamu mwanawe Pravind, waziri mkuu wa nchi hiyo, ambaye alishinda muhula wa miaka mitano ijayo kufuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwaka 2019.

Jugnauth, alizaliwa Machi 29, 1930, ambapo alianza harakati za siasa mnamo mwaka 1963 alipochaguliwa kuwa mbunge.

Mnamo mwaka 1965, Jugnauth alishiriki katika mkutano wa kihistoria huko London ambao ulifungua njia ya kupitishwa kwa katiba katika koloni hilo la Uingereza wakati huo, ambapo ilikuwa chachu ya kupata uhuru miaka mitatu baadaye.

Siku zote alikuwa akifanya kampeni kali ya kuwa na Visiwa vya Chagos, eneo la Uingereza nje ya nchi hiyo iliyo katika Bahari ya Hindi.

Katika miaka ya chini ya utawala wake, Mauritius iliendelea kutoka uchumi duni, unaotegemea kilimo na kuwa moja ya nchi tajiri zaidi Afrika, muujiza ambao mara nyingi huhusishwa na Jugnauth.

Waziri Mkuu Narendra Modi wa India, rafiki wa karibu wa kisiwa hicho, alimsifu “mbunifu wa Mauritius katika nyanja za kisasa” katika ujumbe wake wa pole alisema kuwa kiongozi huyo alistahili sifa kwa kuifanya nchi hiyo kupiga hatua ya kiuchumi.