NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya Soka ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), imeitambia timu ya ZURA kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana kiwanja cha Wazee Maisara.

Katika mchezo huo miamba hiyo ilionekana kukamiana na kufanikiwa kwenda mapumziko kukiwa hakuna ambae aliuona mlango wa mwenziwe.

Kipindi cha pili kilipoanza ndicho kilichotoa majibu ya nani ataibuka na pointi tatu baada ya ZECO kupitia kwa mchezaji wake Faridi Juma Mabrouk kuifungia timu yake dakika ya 65.