MILAN, Italia
KLABU ya Paris St-Germain imemsajili beki wa kulia, Achraf Hakimi kutoka Inter Milan kwa mkataba wa miaka mitano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco mwenye umri wa miaka 22, alikuwa pia akihusishwa na Chelsea ambayo ilitaka kumjumuisha beki wa pembeni, Marcos Alonso katika makubaliano yoyote yanayowezekana.

Hakimi amefunga magoli saba na akaokoa pasi nane za msaada msimu uliopita akiisaidia Inter kutwaa taji lao la kwanza la ‘Serie A’ tangu 2010.
“Ninajisikia fahari kubwa,” alisema.

“Baada ya Hispania, Ujerumani na Italia, Paris St-Germain inanipa nafasi ya kugundua ubingwa mpya na moja ya klabu maarufu duniani”.

Hakimi alianza soka yake huko Real Madrid na alifurahia miaka miwili ya mkopo na Borussia Dortmund kabla ya kujiunga na Inter mnamo 2020.Ndiye usajili mpya wa kuvutia uliofanywa na PSG ya Mauricio Pochettino, ambaye alikosa ubingwa wa ‘Ligue 1’ mwaka jana mbele ya Lille, baada ya kuwasili kwa Georginio Wijnaldum kwa uhamisho wa bure kutoka Liverpool.(AFP).