DHAKA, BANGLADESH

TAKRIBAN watu 52 wamefariki na wengine wapatao 26 kujeruhiwa baada ya moto mkubwa kuteketeza kiwanda cha kutengeneza chakula na vinywaji cha Hashem kilichopo eneo la Rupganj nje ya mji mkuu wa Bangladesh.

Taarifa kutoka kwa maafisa wazima moto zinasema kuwa moto huo ulianza usiku wa kuamkia juzi, katika jengo hilo la ghorofa tano.

Awali polisi ilisema watu watatu wamefariki lakini baadaye waligundua miili ya watu baada ya moto huo kuzimwa.

Hapo awali, familia zilitofautiana na polisi kwa kulalamikia kutoarifiwa chochote kuhusu hatma ya wapendwa wao.

Habari kuhusu ni watu wangapi waliokuwa kwenye kiwanda hicho na wangapi hawajulikani walipo hazikupatikana. Serikali ya Bangladesh imeamuru kuanzishwa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha moto huo.