LONDON, England
KLABU ya Tottenham Hotspurs imefikia uamuzi wa kumuuza mlinzi wake wa kati raia wa Ubeligiji, Toby Alderweireld Al-Duhail ya Qatar.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyejiunga na Spurs mwaka 2015, amesafiri kwenda jijini Doha na inaelezwa kuwa utambulisho wake unategemewa kufanyika wiki ijayo.

Toby anaondoka klabuni hapo baada ya mechi 236 kwenye viunga vya London akitokea Atletico Madrid, mkataba wa beki huyo ulitakiwa ufike kikomo 2023, lakini, klabu hiyo ipo kufanya usafi wa wachezaji kupata sura mpya chini ya kocha, Nuno Espirito Santo pamoja na Mkurugenzi wa Michezo, Fabio Paratici.(Goal).