TOKYO, JAPAN

MNYANYUA uzito wa Uganda amepatikana siku nne baada ya kutoweka kwenye kambi ya mazoezi ya Olimpiki huko Japan akiwa ameacha barua ilioandika kuwa anataka kufanya kazi.

Kukimbia kwa Julius Ssekitoleko kuambatana na wakati wa wasiwasi mkubwa kwa umma juu ya hatari za virusi vya corona ikiwa maelfu ya wageni wanawasili kwa Michezo hiyo.

“Amepatikana katika jimbo la Mie akiwa hana majeraha na wala haja husika na uhalifu wowote,” alisema ofisa wa polisi wa Osaka, ambaye alikataa kutajwa jina.

Taarifa zilizotolewa siku ya ijumaa baada ya Ssekitoleko kushindwa kujitokeza kwa uchunguzi wa coronavirus na hakuwa kwenye chumba chake cha hoteli.

Inaelezwa kuwa mwanamichezo huyo wa miaka 20 aligundua kuwa  hivi hataweza kushindana kwenye Michezo ya Tokyo, kwa sababu ya mfumo wa upendeleo.