NA JOSEPH NGILISHO ARUSHA
JESHI la Polisi mkoa wa Arusha, linamshikilia Melita Ndaletyan (34) kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja kaka yake Kiseri NdaIetyan ( 38), baada ya marehemu kumzuia mtuhumiwa aliyekuwa akitaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yao mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Justine Maseju, tukio hilo lilitokea Jana majira ya saa 6:30 usiku, katika Kitongoji cha Naamalasin, Kata ya Noondoto wilayani Longido mkoa wa Arusha.
Alidai kuwa Kiseri alifariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mdogo wake ambapo wote wawili ni wafugaji na ni ndugu wanaoishi boma moja na kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitaka kuzini na mke wa kaka yake ambaye hakuwepo nyumbani wakati huo.
Kamanda amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kutaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake na kuzuiwa na marehemu kufanya jambo hilo jambo lililosababisha ugomvi kati yao.
“Mtuhumiwa, marehemu pamoja na kaka yao mwingine wote walikuwa wanaishi kwenye boma moja hivyo mtuhumiwa wakati anataka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake (mkubwa) ambaye hakuwepo nyumbani, marehemu alitokea na kumkataza kufanya hivyo ndipo mtuhumiwa alimchoma na kitu chenye ncha kali,”