ADISS ABABA, ETHIOPIA

MAMLAKA nchini Ethiopia katika eneo la Amhara imesema watafungua mashtaka dhidi ya jeshi la majirani zao wa Tigray.

Inaelezwa kuwa waasi wamechukua maeneo mengi ya Tigray katika wiki za hivi karibuni, na vikosi vya nchi hiyo pamoja na washirika wake kuondoka katika maeneo muhimu.

Msemaji wa serikali ya Amhara imesema uvumilivu unawashinda.Wajumbe wa zamani wa usalama wametakiwa kujitolea na kuhamasisha.

Vikosi vya Tigray vikiwa vinaelekea katika eneo la Amhara katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, huku pande zote mbili zikiona kuwa na haki sawa.

Inaonekana kuwa kuna ari kubwa ambayo inaweza kusababisha damu kumwagika tena na kuanzisha awamu nyingine ya mgogoro.

Hapo awali Ethiopia ilikuwa nchi imara katika Pembe la Afrika na mshirika muhimu wa Magharibi katika vita dhidi ya ugaidi. Hivyo iko hatari ya kuongezeka kwa vita zidi na kuwa taifa dhaifu barani Afrika.