BAMAKO, MALI
MTU ambae anatuhumiwa kufanya jaribio la kutaka kumuua rais wa mpito wa taifa hilo, Assimi Goita, amefariki akiwa katika mikono ya polisi.
Mtuhumiwa huyo ambae utambulisho wake haujawekwa wazi, aliwekwa kizuizini baada ya jaribio la mauaji la katika sala ya Eid al-Adha iliyofanyika katika msikiti mkuu mjini Bamako.
Katika taarifa yake serikali ya Mali ilisema afya ya mtuhumiwa huyo ilianza kuzorota, alipelekwa hospitali lakini baadae akafariki dunia.
Serikali ilisema kumetolewa agizo la kuchunguza kiini cha kifo hicho.