NA MWANAJUMA MMANGA

JESHI la polisi Mkoa wa Kusini Unguja, linaendelea kumtafuta mtuhumiwa Issa Twahir Issa (29) mkaazi wa Kizimkazi Mkunguni kwa tuhuma ya kumshambulia kwa mapanga Ali Rashid Simai (18) mkaazi wa Kizimkazi Mkunguni huko Baa ya Kalbonia iliyopo Kizimkazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo Suleiman Hassan Suleiman akithibitisha kutokea kwa tukio hilo. alisema tukio hilo limetokea  Mey 17, mwaka huu majira ya saa 7:00 za mchana huko baa.

Alisema mtuhumiwa huyo alimshambulia kwa mapanga Issa katika sehemu zake za kichwa, mguu wa kulia na kutenganisha   kiganja cha mkono wa kulia na kumuumiza vibaya sana huku alitenda kosa hilo akijua kuwa ni kosa la kisheria.

Aidha, alisema kijana Issa alikuwa na silaha hizo huku alikuwa akishambuliana kwa matusi kijana Ali ambapo chanzo cha ugonvi huo bado hakijajulikana na yupo hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya kuptiwa matibabu.

Alisema Kamanda Suleiman, kijana Issa bado jeshi la polisi linaendelea kumsaka na akipatikana hatua kali atachukuliwa dhidi yake.

Hivyo, Kamanda Suleiman, ametoa wito kwa vijanakucha tabia ya kujichukulia hatua mikononi mwao na kuwaomba kupeleka malalamiko katika vyombo vya sheria.