NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Azam FC, umeendelea kufanya usajili wa wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi chao.

Baada ya kusajili wachezaji watatu hivi karibuni juzi  wameongeza mchezaji mwingine wa kimataifa kutoka nchini Kenya Kenneth Muguna.

Mchezaji huyo amemwaga wino kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili.

Muguna alikuwa akiitumikua Gormahia ya nchini Kenya ambayo pia alikuwa akiitumikia kipa Mtanzania wa Azam David Kisu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Azam FC Keneth Mguna ni mchezaji bora wa kombe la shirikisho nchini humo, ambapo Gormahia waliibuka mabingwa kwenye michuano hiyo.