ZASPOTI
KARIM Benzema, atasalia Real Madrid hata kama klabu hiyo ya Hispania itafanikiwa kumsaini mshambuliaji mwenzake wa Ufaransa, Kylian Mbappe, kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto.
Si rahisi kupata mshambuliaji katika historia ya Real Madrid ambaye amecheza michezo mingi kuliko Benzema. Ni Carlos Gonzalez ‘Santillana’ tu aliyecheza mara nyingi kwenye klabu hiyo michezo 654 kuliko mechi 559 za Benzema.
Ni miaka 12 tangu Mfaransa huyo ajiunge na ‘Los Blancos’, na hakika imekuwa na safari ya mafanikio. Klabu hiyo ilimuweka kwenye orodha ya uhamisho mara kadhaa katika miaka yake ya kwanza, lakini, bado amebakia Madrid.
Bila ya Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, Benzema imekuwa kituo kikuu cha Real Madrid. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, alimaliza msimu wa 2020/21 na idadi ya pili ya mabao kwenye kazi yake baada ya kucheka na nyavu mara 30.
Benzema pia alifunga mara nne kwenye Euro 2020, ambapo aliwazidi, Kylian Mbappe na Antoine Griezmann na kumaliza bao moja tu nyuma ya Cristiano Ronaldo, Harry Kane, Romelu Lukaku na Emil Forsberg.
Bila ya kujali kama Mbappe atafika msimu huu wa joto au la, Benzema bado atakuwa kiongozi wa safu ya kushambulia wa timu hiyo.(Marca).