NA VICTORIA GODFREY

TIMU ya Bilioni Paint,Black Six  zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya mashindano ya soka ya Ndondo cup  .

Bilioni imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Twiga uliocheza juzi kwenye Uwanja wa Bandari ,hivyo   imeongoza  kwa pointi saba ,huku Black Six wametoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Sinza Star  iliyochezwa Urafiki ,hivyo kujikusanyia  pointi tano katika  michezo wa mwisho ya hatua ya 32.

Timu nyingine zilizopata nafasi  Tabata All Star ikiwa na pointi sita,Uruguay pointi sita ,Sisi kwa Sisi na Keko Furniture.

Akizungumza na Zanzibar leo Katibu wa mashindano hayo Daud Kanuti,alisema  imebaki michezo michache kukamilisha  hatua ya timu 32 ya mashindano hayo.

Alisema kuwa timu zitakazofanya vyema katika michezo yao ya mwisho zitapata nafasi ya kufuzu na kuingia  hatua 16 bora.

Alitoa wito kwa mashabiki kujitokeza kushangilia  na kuzingatia na kufuata taratibu za kuchukua tahadhari ya kujikinga na virusi vya Covd- 19.