WASHINGTON, MAREKANI

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amekutana na Mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus Kuwait na kuahidi uungaji wake mkono kwa uchunguzi wa shirikia hilo kuhusu chanzo cha janga la virusi vya corona.

Katika taarifa ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price, inasema Blinken alisisitiza hitaji la awamu mpya ya uchunguzi ambayo itafanyika kwa wakati, yenye kujikita katika ushahidi, uwazi, kuongozwa na wataalam na pasipo kuingiliwa.

Shiria hilo la afya duniani lipo katika shinikizo kali la uchunguzi mpya na wa kina wa namna gani ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo vya takribani milioni nne duniani kote ulivyozuka.

Januari ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, WHO iliweza kuipeleka timu huru ya wataalamu wa kimataifa mjini Wuhan, kwa shabaha ya kuwasaidia wenzao wa China kulisaka jawabu hilo.