KINSHASA, DRC

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi na mwenzake wa Burundi Évariste Ndayimishiye, wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kwa maslahi ya nchi hizo jirani.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mazungumzo ya viongozi hao wawili yaliyofanyika jijini Kinshasa, kufuatia ziara ya rais Ndayishimiye nchini DRC iliyofanyika mwanzoni mwa wiki hii.

Ziara hiyo ya rais Ndayishimiye jijini Kinshasa, ni jitihada za rais Tshisekedi, kuimarisha ujirani mwema, baada ya wiki kadhaa zilizopita, kukutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni na Paul Kagame wa Rwanda.

Viongozi hao walikutana kwa saa mbili ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuhusu kushirikiana kwenye suala usalama baina ya nchi zao na pia walijadili ujenzi wa reli kati ya nchi hizo mbili.

Rais Evariste Ndayimishiye alielezea umuhimu wa nchi hizo mbili, kuimarisha mahusiano yao na kushirikiana kwenye masuala ya maslahi ya Burundi na DRC.

Mwezi Oktoba mwaka 2020, jeshi la DRC liliripoti kuwaondoa wapiganaji wa FNL kutoka Burundi katika kambi zao katika mkoa wa Kivu Kusini.

Aidha, Ndayishimiye alisema nchi yake iko tayari kuwapokea raia wa nchi hiyo waliokimbilia nchini DRC.

DRC inapafa hifadhi ya ukimbizi watu zaidi ya 45,000 kutoka Burundi waliokimbia nchi yao kufuatia mgogoro wa kisisa uliibuka mwaka 2015 baada ya hyati rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu, kulingana na wapinzani wake.