Limetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu
RAIS wa Marekani katika zaira zake za ndani na nje ya nchi hutembea kwa kubebwa na gari Cadillac ambapo kwa kawaida gari hilo hujulikana kwa jina maarufu la BEAST ama mnyama mkali.
Gari hiyo imepewa jina hilo kutokana na kusheheni mifumo mbalimbali ya kujilinda dhidi ya jaribio la mashambulizi kwenye msafara wa rais wa Marekani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari za Cadillac zinatengenezwa kwa kampuni kubwa ya kutengeneza gari ya nchimi Marekani ya General Motors, ambapo inakisiwa kuwa gari hiyo ina thamani ya dola millioni 15.8.
Inasemekana mifumo ya gari anayopanda rais wa Marekani ni siri kubwa, japo linasemekana kuwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya mashambulizi mbalimbali ya risasi na makombora.
Aidha gari hiyo ina vifaa vya huduma ya afya kwa rais ikiwemo ikiwemo mashine inaweza kutoa hewa ya oksijini na kwamba inatajwa kama moja ya gari salama zaidi duniani.
Cadillac ina uzito wa takriban kilo 9000 ambalo kila mara rais anapokuwa katika ziara ya kigeni husafiriswa na ndege ya Airfoce One na kusimamiwa na kitengo cha ujasusi cha Marekani.
Rais anapokuwa katika ziara ya kigeni husafiriswa na ndege ya Airfoce One na kusimamiwa na kitengo cha ujasusi cha Marekani limedaiwa kumiliki vipengele vinavyoweza kumlinda rais wa taifa hilo lenye uwezo mkubwa duniani iwapo kutatokea shambulizi.
Kwa ufupi kabisa gari inayombeba rais wa Marekani sio gari la kawaida na moja kwa moja unaweza kusema kuwa hilo ni gari la kivita.
Kwa nje gari hiyo imeundwa kwa kutumia vyuma vilivyochanganywa na aluminium, titanium na ceramic vyenye uzito wa nchi sita kuzuia risasi yoyote kuingia.
Bodi ya gari hilo limejengwa kwa ujazo wa nchi sita ambao una uwezo wa kuhimili shambulio la bomu, ambapo milango ya gari hilo, ina uzito wa nchi 8 na inapofungwa ina uwezo wa kuwalinda asilimia 100 wale walio ndani ya gari hilo iwapo kutatokea shambulio la kemikali.
Milango hiyo pia inaweza kuwekwa umeme ili kuwazuia wanaotaka kuingia kwa lazima, huku madirisha ya gari hilo yana safu tano za vioo vinavyoweza kuzuia shambulio la risasi.
Ni dirisha la dereva pekee ndilo linaloweza kufunguka, lakini kwa nchi tatu pekee, shina la gari hilo limejengwa na chuma kinachoweza kulilinda dhidi ya shambulio la bomu.
Matairi yake hayawezi kupata pancha au kutoboka yakiwa na chuma ndani yake, hatua hiyo huliwezesha gari hilo kuendelea na safari yake hata iwapo matari hayo yameharibiwa.
Kwa upande wa nyuma gari hilo lina uwezo wa kumwaga mafuta yanayoteleza barabarani ili kuyakosesha udhibiti magari yanayolifukuza.
Eneo la ndani ya gari la ”The Beast” linimiliki vipengele kadhaa vya kujilinda, ikiwemo kipengee kimoja ambacho kinaweza kukwepa shambulio la kemikali kulingana na Reuters.
Eneo la nyuma la gari hilo ndilo ambalo rais na abiria wengine wanne hukaa likiwa limezibwa kwa vioo na ni rais pekee aliye na uwezo wa kushusha vioo vya gari.
Gari hilo pia lina kitufe cha kukabiliana na hofu pamoja na usambazaji wa oksijeni.
Kiti cha rais kilichopo nyuma ya gari hilo kinamiliki simu ya setlaiti yenye mawasiliano ya moja kwa moja na makamu wa rais wa taifa hilo na makao makuu ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo The Pentagon.
Tangi la mafuta la gari hilo limejengwa na mabati ambayo yanaweza kuzuia shambulio na kujazwa mapovu maalum ambayo yanalizuia gari hilo kulipuka iwapo litapata ajali.
Eneo la nyuma la gari hilo (Boot) lina mfumo wa kukabiliana na moto, vitoa machozi na linaweza kutoa skrini yenye moshi.
Vilevile gari hilo lina dereva ambaye amepata mafunzo maalum ya kukabiliana na hali ya kutatanisha na kutoroka na rais. Gari hilo pia linamiliki bunduki fupi na bomba la kutoa gesi ya kutoa machozi.
Mifuko ya aina ya damu ya rais pia huwa ndani ya gari hilo iwapo atahitaji kuwekwa damu pale dharura itakapotokea ikiwemo ajali ama tatizo jengine la kiafya.
Eneo la mbele la dereva lina kituo cha mawasiliano na mfumo wa ufuatiliaji wa GPS, vilevile kuna kamera iliofichwa inayoweza kuona matukio mbalimbali nyakati za usiku.