BEIJING, CHINA

CHINA imepeleka ndege ili kuwaondoa raia wake 210 walioko nchini Afghanistan baada ya majeshi ya kimataifa yaliyoongozwa na Marekani kuondoka nchini humo

Gazeti la China Global Times limearifu kwamba ndege ya China iliondoka mjini Kabul wiki iliyopita na kuwapeleka raia wa China kwenye mji mkuu wa jimbo la kati la Hubei.

Kampuni za China zimewekeza vitega uchumi katika sekta za migodi na miundombinu nchini Afghanistan lakini rasilmali hizo zinakabiliwa na hatari wakati amabapo kundi la Taliban linaendelea kuyachukua maeneo mengi nchini Afghanistan hali ambayo inauweka mji mkuu wa Kabul katika hatari.

Masuala ya usalama ya Afghanistan yatajadiliwa kwenye mkutano wa wiki ijayo wa shirika la ushirikiano la Shaghai linalozijumuisha nchi kadhaa ikiwa pamoja na China na Urusi.