NA ASIA MWALIM

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamesema uongozi mzuri ni pale viongozi wa juu wanaposhuka kwa wanachama wa chini kuzungumza nao mambo mbalimbali ya chama na maendeleo.

Walisema kufanya hivyo ni kunufaisha chama hicho kuendelea kubaki madarakani sambamba na kutatua changamoto za wanachama wa ngazi za chini ambao wananafasi ya kulivusha jahazi la CCM.

Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti walipokua wakizungumza na Zanzibarleo, kufuatia ziara, nasaha alizotoa Katibuu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Godfrey Chongolo.

Aidha walisema Ujio wa Katibu Mkuu Taifa kufika  Zanzibar na kushuka kwa wanachama wa chini ni kufuata kanuni na ilani ya CCM, hivyo ni wazi amedhihirisha utendaji wa majukumu yake.

Hemed Ali Sleiman, alisema, wamefurahishwa na hatua ya kuwafikia wanachama, kusema mikakati yake, ili Kukipa msukumo chama kiendelee kusonga mbele na kuwapa imani wanachama wadogo.

Aidha, alisema tangu kuchaguliwa nafasi ya Mwenyekiti Mama Samia, ni mara ya kwanza kukutana wana CCM kwa wingi kiasi hicho kiasi kwamba kila mwanachama alifurahishwa na mazungumzo ya Katibuu huyo, yameleta faraja, kujifunza namna ya uongozi bora na kuwafanya wanachama hao kupata nguvu na msukumo zaidi.