CONAKRY, GUINEA
TAKRIBANI miaka miwili baada ya zaidi ya wanasayansi 10,000 kutoka mataifa 150 kutangaza dharura ya kushughulikia athari za mabadiliko ya tabia nchi, wameurejea tena wito wao na kutaka uharaka wa utatuzi wa kitisho hicho.
Kwa mujibu wa jarida la kisayansi la BioScience, wanasayansi hao walisema mabadiliko yanahitajika haraka sana kwa kuulinda uhai na dunia.
Azimio lililosainiwa awali na wanasayansi 11,000 kwa sasa limeongezewa nguvu na saini nyengine 2,800.
Tangu kusainiwa kwake kwa mara ya mwanzo azimio hilo la dharura la kimazingira 2019, kumetokea majanga kadhaa ya mafuriko, majanga ya moto ya misituni na ongezeko la joto, jambo ambalo linaonesha wazi ongezeko la athari za kimazingira duniani.