NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya Gando United imeondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jadida Heroes, ikiwa ni muendelezo wa ligi daraja la pili Mkoa wa Kaskazini Pemba hatua ya sita bora.

Mchezo huo uliokuwa wa ushindani ambao ulitimua vumbi uwanja wa FFU Finya majira ya saa 10:00 jioni.

Hadi timu hizo zinatoka uwanjani kipindi cha kwanza, Gando ilikuwa ikiongoza kwa bao moja lililofungwa na Khamis Ali dakika ya tano.

Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko kurekebisha makosa yaliojitokeza katika kipindi cha kwanza.

Marekebisho yalileta mafanikio kwa Gando katika dakika ya 73 na 90 Mbaraka Maulid alipofunga mabao mawili na kusimama hadi mwisho wa mchezo huo.