LONDON, England

OLIVIER Giround amekamilisha dili lake la usajili ndani ya AC Milan inayoshiriki Serie A akitokea klabu ya Chelsea inayotumia Uwanja wa Stamford Bridge kwa mechi zake za nyumbani.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 alifanyiwa vipimo siku ya Ijumaa kabla ya kukamilisha dili hilo ambalo amelifurahia huku ada ya usajili wake ikifichwa.

Giroud, alijiunga na Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England kwa sasa inanolewa na kocha mkuu, Thomas Tuchel kwa dau la pauni milioni 18, Januari 2018 ameshinda taji la FA, Europa League na Mei alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika zama zake za kuitumikia Chelsea.

Nyota huyo amewashukuru viongozi na mashabiki wa Chelsea kwa kuwa naye kwa muda ambao alikuwa hapo huku akibainisha kwamba anahitaji kushinda mataji mengi zaidi ndani ya AC Milan.

Kushinda kwake kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Chelsea kumeongeza thamani yake ambapo kwenye mshahara wake mpya ndani a kikosi cha AC Milan atakuwa anapewa na bonasi

Baada ya kumwaga wino nyota huyo amesema:”Malengo yangu ni kuona kwamba tunashinda mataji mengi zaidi. Hii ndio sababu mimi ninacheza mpira kikubwa ni kuona kwamba ninafanya ushindani,”.