NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya Simba, Didier Gomes Da rosa, amesema malengo yao ya kuchukua ubingwa bado yapo pale pale.

Simba juzi walipoteza pointi tatu dhidi ya Yanga kwa kuruhusu kufungwa bao 1-0 mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mpaka sasa Simba wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 73, wamebakisha michezo miwili ili kuweza kutangaza ubingwa.

Akizungumza na vyombo vya Habari juzi, Gomez alisema mchezo wao dhidi ya Yanga sio mwisho wa malengo yao kwani ni moja ya michezo ya ligi.

Alisema wanachokihitaji ni kubeba ubingwa wa ligi na kuhakikisha wanafanya vizuri katika kila mchezo uliopombele yao ili kubeba taji hilo la msimu huu.

“Ni kweli mchezo wetu na Yanga tulipoteza lakini huo ni mchezo wa ligi kama ilivyo michezo mingine, malengo yetu hayajabadilika tunaendelea kuutafuta ubingwa,” alisema.

Simba Julai 7, mwaka huu watavaana na kikosi cha KMC katika mchezo wao wa 31 wa ligi hiyo.