NA MWANAJUMA MMANGA

WATU wawili wamefariki dunia kwa matukio mawili tofauti likiwemo la uunywaji wa pombe ya Kienyeji (Gongo) huko Mkoa wa Kusini Unguja.

Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Suleiman Hassan Suleiman, akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, na kuwataja marehemu hao ni Feisal ambae jina la baba halijafahamika anaekisiwa kuwa anauri wa miaka (25), Mkaazi wa Mwanakwerekwe na Bryan  Peter Adriano (7)mkaazi wa Jozani amefariki kwa kugongwa na gari huko Kikungwi.

Suleiman alisema, tukio la kwanza linalomuhusisha Feisal alisema tukio hilo  limetokea majira ya saa 4:00 za asubuhi huko Kikungwi Mkoa huo, Marehemu alitoka nyumbani kwao Mwanakwerekwe na kwenda Kikungwi na alipofika maeneo yanayouzwa pombe ya kienyeji iitwayo Gongo ndipo yalipotokea mauti yake.

Alifahamisha kuwa baada ya marehemu huyo kupatikana na  wasamaria wema na kuchukuliwa kufikishwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajili ya uchunguzi.

Aidha, Kamanda Suleiman, alisema uchunguzi umebainika marehemu amekunya pombe nyingi na kali na kupelekea kifo chake na baadae kukabidhiwa jamaa zake.

Hivyo Kamanda Suleiman aliwataka wauzaji kuacha kujishughulisha na biashara hiyo kwani itawaathiri vijana wengi kupoteza maisha ambao ndio nguvu kazi wa baadae.

Alisema tukio la pili la ajali ya gari iliyouwa  Bryan na  kumgonga gari  Mwenda kwa Miguu mnamo Juni 6, mwaka huu majira ya saa 5:40 asubuhi huko Kitogani.