BLOEMFONTEIN, AFRIKA KUSINI

WAZIRI  Mkuu wa KwaZulu-Natal, Afrika Kusini ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo liloathiriwa zaidi na vurugu mbaya zilizotokea mapema mwezi huu.

Sihle Zikalala alisema kwamba hatua hiyo itaruhusu kipaumbele kuelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu na kuinua uchumi wa jimbo hilo, pamoja na kushughulikia mvutano uliojitokeza miongoni mwa wakaazi.

Mnamo mwezi Julai, majimbo ya KwaZulu-Natal na Gauteng yalikumbwa na ghasia kubwa zilizosababisha zaidi ya watu 300 kufariki dunia pamoja na uporaji wa biashara na uharibifu wenye thamani ya mamilioni ya dola.