HUKU nchi za Afrika zikihangaika kupambana na janga la corona, wakati huo huo taarifa zinaeleza kuwa bara hilo limeathirika sana na harakati za vitendo vya kigaidi.

Makundi ya kigaidi yaliyoenea katika maeneo na nchi mbalimbali yanasababisha fadhaa kwa baadhi ya nchi za Afrika na wananchi wake.

Kwa mfano, kuna kundi la Boko Haram katika nchi nyingi za Afrika ya Magharibi, ukiongozwa na Nigeria na pia kundi la Al-Shabab huko Afrika ya Mashariki, hasa katika Somali, na mashambulio ya Al-Qaeda huko Afrika ya Kaskazini, vinazuia kuwepo amani na usalama nchini.

Hakuna shaka kuwamba kuna changamoto na matatizo yanayoyakabili bara la Afrika na kuzuia katika harakati zake za kuelekea maendeleo ya bara hilo kwa nyanja zote za kiuchumi, kielimu, kisiasa na kijamii pia.

Na umuhimu wa vikwazo hivi ni kuenea makundi ya kigaidi katika kote Afrika, na jambo hili limeibua wasiwasi nyingi, sio tu kwa kiwango cha viongozi wa bara hilo, lakini pia katika kiwango cha mashirika ya kimataifa.

Katika miaka ya mwishoni, nchi za Afrika zimefanya juhudi kubwa kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi yaliyokuwepo kwenye nchi zao, lakini kumeshuhudiwa kuongezeka kwa makundi haya mapya ya kigaidi.

Machafuko ya kisiasa, udhaifu wa serikali za Kiafrika katika kupambana na makundi hayo, kuhitaji zaidi kwa vikosi vya kijeshi, na kutokuwepo ushirikiano kuhusu masuala ya usalama na ya kijeshi, mambo yote hayo yamezuia mafanikio ya nchi hizi katika vita vyao dhidi ya makundi ya kigaidi.

Kutoka na kuongezeka kwa harakati za vitendo vya kigaidi barani Afrika, baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliunda timu maalum kwa ajili ya kuangalia kitisho cha usalama barani humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya timu hiyo iliyowailishwa na wataalamu wa umoja huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imeeleza kuwa makundi ya kigaidi yameeneza shughuli zao katika maeneo ya magharibi na mashariki mwa Afrika.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa makundi hayo yana uwezo mkubwa wa kujidhaminia fedha na kutumia silaha za kisasa ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kigaidi.

Timu hiyo ilisema kuwa matawi yanayofungamana na makundi ya ugaidi yamejizatiti katika maeneo ya Afrika ya Kati, Sahel, magharibi na mashariki kwa Afrika na hasa nchini Somalia ambayo kwa sasa haina serikali kuu yenye nguvu.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuenea makundi ya kigaidi barani Afrika kwa hakika imeweka wazi ongezeka kubwa la shughuli za makundi ya kigaidi katika bara hilo na hasa eneo la Sahel, ambalo limekuwa uwanja na maficho makuu ya makundi ya Daesh na al-Qaida pamoja na matawi yake barani humo.

Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, mashambulizi yaliyofanywa na makundi hayo yameongezeka karibu mara 20 na waathirika wameongezeka kwa zaidi ya mara tisa.

Suala la kuongezeka ugaidi na misimamo ya kupindukia mipaka katika eneo la Sahel limetokea kuwa tatizo kubwa katika eneo hilo kwa kadiri kwamba ni miaka mingi sasa ambapo majeshi na polisi ya nchi za eneo hilo na hasa Mali, Niger na Burkina Faso yamekuwa yakitumia fedha na muda wao mwingi kupambana na makundi hayo.

Kuna sababu kadhaa tofauti ambazo zimechangia tatizo hilom moja ya sababu hizo ni kuwa eneo hilo lina mambo mengi yanayochangia vijana kujiunga na makundi ya kigaidi.

Kwa kawaida vijana hao masikini huwa kwenye hali mbaya ya kimaisha na hivyo huathirika haraka na hadaa za kutajirika haraka, zinazotolewa na makundi ya kigaidi.

Sababu nyingine ni kutokuwepo maendeleo ya kutosha kiuchumi, kijamii na kimiundombinu katika nchi nyingi za Afrika na hasa zile zilizopo katika eneo la Sahel.

Sababu hiyo imesababisha vijana wengi kuhatarisha maisha yao kwa kuamua kusafiri kimagendo kuelekea nchi za Ulaya kupitia nchi za kaskazini mwa Afrika, hasa Libya.

Kukataa tamaa maishani kumewafanya vijana wengi katika nchi hizo kushawishiwa kirahisi na makundi ya kigaidi na hivyo kubeba silaha dhidi ya raia na serikali zao dhaifu na hatimaye kuharibu zaidi hali ya mambo katika nchi hizo.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema, kuenea kwa makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel na hasa katika nchi za Mali, Burkina Faso, Ivory Coast, Niger, Senegal, Nigeria, Chad na Cameroon kumeongeza wasi wasi na hofu kubwa katika nchi hizo.

Wanasema makundi yanayofungamana na Daesh na al-Qaida sasa yameimarisha shughuli zao katika eneo la mashariki mwa Afrika tokea Somali hadi Kenya na Tanzania hadi Msumbiji.

Suala ambalo limezua wasi wasi kuhusiana na mapambano dhidi ya ugaidi barani Afrika ni uwepo barani humo wa nchi za Magharibi na hasa Ufaransa na Marekani kwa madai ya kupambana na ugaidi.

Licha ya kuwa Ufaransa ilituma askari wake huko Mali miaka minane iliyopita kwa kisingizio cha kupambana na tishio la makundi ya kigaidi kama Daesh na al-Qaida lakini Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo alisema siku chache zilizopita kwamba nchi yake sasa imeamua kusitisha operesheni hiyo na kwamba itapunguza idadi ya askari wake walioko nchini humo ambao wanafikia elfu 5 hadi nusu.

Licha ya miaka mingi ya madai ya kupambana na makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel, Ufaransa si tu kwamba haijapata mafanikio yoyote katika uwanja huo bali imechochea zaidi shughuli za makundi hayo katika eneo hilo.

Nchi hiyo sasa inaitika Marekani itume askari wake katika eneo hilo kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Pamoja na hayo ni wazi kuwa makundi ya kigaidi yanaendelea kuongeza shughuli na wanachama wao barani Afrika na hasa katika eneo la Sahel.

Jordan Koop, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anaashiria shughuli za makundi ya kigaidi barani Afrika na hali mbaya ya bara hilo katika nyanja za uchumi, siasa na usalama na kusema: Katika siku zijazo kutatokea vita vikubwa dhidi ya ugaidi na wala ASia Magharibi hakitakuwa tena kitovu muhimu cha mapambano dhidi ya fikra na mielekeo ya kupindukia mipaka.