Na Sheikh Kamal Abdul Waheed (Kituo cha kiislamu cha Misri (DAR)
Humfanya kuwa karibu na Mola wake
HAKIKA ya hija ni faradhi miongoni mwa faradhi za (Mwenyezi Mungu) Uislamu na ni fungu miongoni mwa mafungu ya imani na ni alama miongoni mwa alama za dini ya Mtume (SAW) nayo ni mkutano mkubwa wa dunia wanakusanyika hapo waislamu wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu toka pande zote za dunia.
Na amesema kweli Mwenyezi Mungu pale aliposema (Na watangazie watu hija watakuja wenda kwa miguu toka sehemu mbalimblai za dunia).
Hii hakika amefaradhisha Mwenyezi Mungu kwa wale wenye uwezo katika umati wa Mtume Mwaminifu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Ni miliki yake Mwenyezi Mungu kwa watu wajibu wa kuhiji katika nyumba kongwe kwa mwenye kuweza kwa njia zake na atakayekufuru hakika Mwenyezi Mungu ni tajiri kwa viumbe)).
Maana hii amesisitiza Mtume (SAW) kwa maneno yake kwa yale aliyoyatoa imamu muslim toka kwa Abii Hurairata, amesema (Ametuhutubia Mtume (SAW) akasema (Enyi watu hakika amefaradhisha Mwenyezi Mungu kwenu hija hivyo hijini) mtu mmoja akasema: Jee ni kila mwaka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?
Akanyamaza, hadi akasema hivyo mara tatu, akasema Mtume (SAW) laity ningesema (Ndiyo) basi ingewajibishwa na wala msingweza fanyeni yale niliokuachieni kwa hakika wameangamia waliopita kabla yenu kwa wingi wa masuali yao na kutofautiana kwao na manabii wao pale nitakapo waamrisheni jambo lifanyeni kwa kadri muwezavy na nitakapowakatazeni jambo basi liacheni.
Basi hija ni faradhi ya mara moja tu katika umri ni wajibu kwa mwenye uwezo mara moja isipokua kama mtu atajiongeza yeye mwenyewe basi kama ni nadhiri ni wajibu kutekeleza nadhiri hiyo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Kisha wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao na waizunguke sana nyumba kongwe) (29) Haji.
Hakika hija huisafisha nafsi kutokana na uchafu na kuondoa makosa na madhambi ameitoa imamu Bukhari toka kwa Abii Hurairata.
Amesema (Amesema Mtume (SAW) (yeyote mwenye kuhiji nyumba hii na hakufanya maasi wala jambo baya basi atarudi nyumbani kwake kama siku alivyozaliwa na mama yake Kisha hija iliyokubaliwa humuwezesha mwenda hija kuingia peponi hivyo ni ibada ya kujisfaisha na kujilinda na ufakiri, ameitoa Tirmidhi toka kwa Bin Masoud.
Amesema Mtume (SAW) (fatilizeni biana ya hija na umra kwani hizo mbili humkinga mtu na ufakiri na madhambi kama inavyozuia gilisi kutu ya chuma na dhahabu na fedha, na itakuwa na malipo ya hija iliyokubaliwa isipokuwa pepo).
Kisha hija ni muonekano wa umoja wa kiislamu na ni alama ya udugu wa kiimani, huuisha upya roho ya kujuana na udugu na mapenzi na huruma, muislamu huona ajabu kubwa katika viwanja vya Maka na katika ardhi ya arafa na katika kutekeleza nguzo, pale anapoyaona mammilioni ya waislamu wamejaa katika kiwanja cha Mwenyezi Mungu toka mataifa mbalimbali na utofauti walugha zao na sura zao na pia maumbile yao.
Hapo ndipo inapokuingia aya ya Mwenyezi Mungu tukufu ikiwa na uwazi wa sura yake na ukubwa wa maana yake (na miongoni mwa dalili za kuwepo kwake ni kuumba mbingu na ardhi na kutofautisha lugha zenu na rangi hakika juu ya hilo ni dalili kwa wenye elimu) Basi kutofautiana lugha na rangi na matamshi na utaifa na dalili nyingine nyingi, basi ni nani amewakusanya na ni nani alyewaita? Na kwa ajili ya naniwanahiji?
Na anamuomba nani na kwa jina la nani wanaloita? Hao wanahiji nyumba moja na wanamuabudu Mola mmoja na wanaomba Mungu Mmoja mmoja na wanaomba mungu mmoja kwa kusema.
(Tumeitikia ewe Mola tumeitikia tumeitikia huna mshirikia tumeitikia hakika sifa njema na neema ni zako na ufalme huna mshirika.
Mwenda hija anajisikia kuihama nyumba ya dunia kutokana na vazi lake kwa kuvua mapambano yake na huacha cheo chake na umaarufu wake na kusahau mali zake na jamii yake na washida wake na uongozi wake na hufunikwa safari yake kwenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na utiifu na upole, hadi hakuna tofauti kati ya rais na raia wala baina ya tajiri na masikini wala waziri na mnyonge bali wote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ni sawa ameitoa imamu Baikhakiyu toka kwa Jabir Bin Abdillah.
Amesema (Ametuhutubia sisi Mtume (SAW) kati kati ya masiku ya kuchanja hotuba ya kuaga akasema.
Enyi watu, hakika Mola wenu ni mmoja na hakika baba yenu ni mmoja, ehe zindukeni hapana utukufu wa mwarabu kwa asiye mwarabu kwa mwarabu kwa mwarabu wala kwa mtu mwekundu au mweusi.
Isipokuwa uchamungu hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni Yule mwenye kumuogopa sana Mungu, Ehe je nimefikirisha; wakasema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Akasema basin a afikishe Yule aliyekuwepo hapa kwa Yule asiyekuwepo hapa) basi hija inatufundisha umoja kwa sura nzuri na kwa maana njema hivyo ubaguzi hauna nafasi wala utaifa wala ufakhari wa ukoo na uzaliwe wala kwa alama za kung’ara wala ukabila wa kifalme bali wote katika kunyenyekea na utiifu uliokamilika hadi ukubalike kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Basi ni kwa nini waislamu wasiungane kama wanavyoungana katika hija yao? Na ni kwa nini isiungane safu yao kama inavyoungana katika viwanja vya Maka? Kwa nioni unatofautisha na umma pamoja na kuwa sheria ya Mwenyezi Mungu ni moja na ina uweoz wa kuwakusanya?
Na ni kwa nini watoto wa umma huu hawaungani wakawa umma mmoja na umma wetu ni mmoja na Mtume wetu ni mmoja na kitabu chetu ni kimoja na kibla chetu ni kimoja kwa hakika ameweka Mwenyezi Mungu katika nyumba yake siri kubwa kwa namna nafsi zinatamani na roho kupendana na moyo kunungunika na vifua kumiminika hapo hii yote ni kwa kujibiwa dua ya Ibrahimu (AS).