NA HAFSA GOLO

ZANZIBAR ni miongoni mwa nchi inayosifika katika mataifa mbalimbali kutokana na utamaduni na  ustaarabu wa watu wake, waliojaaliwa neema ya ukarimu  kwa wageni wanaoingia nchini, jambo ambalo limesaidia kuendelea  kuaminika katika dunia.

Kutokana na hatua hiyo wageni wengi wanaofika visiwani humu wamekuwa wakivutiwa na ustaarabu, ulioambatana na mila na desturi katika mfumo mzima wa maisha ya watu wake. Itakumbukwa kwamba Zanzibar ni nchi ya visiwa iliojaaliwa upepo mwanana na mandhari nzuri yenye  utulivu na bashasha ya watu wake, huku ikisifika kwa mambo mazuri ya asili ikiwemo tamaduni zake.

Kwa muhtaza huo viongozi wa jimbo la Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja, wameona umuhimu wa kuendeleza mikakati ya makusudi ya kuimarisha masuala ya tamaduni kwa vijana jimboni humo.

Bila ya shaka huo ni mwanza mzuri ikiwa utashughulikia kwa kina utasaidia kuleta matokeo chanya kwa vijana hao, juu ya kutunza na kuenzi masuala ya tamadunia za asili.

Ni ukweli usiopingia tamaduni ni miongoni mwa kielelezo tosha kinachochea katika nchi yoyote, kubainisha wazi tabia na silka za watu wake ikiwemo Zanzibar.