NA ASHA MAULD, IMMZ

SERIKALI  ya Zanzibar imekemea vikalli uharibifu wa Maliasil Bahari, kutokana na kuwepo kwa wibi kubwa la uvamizi wa ukataji wa mikoko unaoendelea katika mikoa yote ya Zanzibar hasa katika maeneo ya Bahari.

Kauli hiyo imekuja baada Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayubu Muhammed Mahmoud, hivi karibuni kutoa  agizo kwa Idara ya Maendeleo ya Misitu, kufuatilia uharibifu mkubwa wa Koko uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Jumuia Hifadh ya Bumbwini Shehia ya Makoba Mkoa wa Kaskazini ‘B’ Unguja.

Akiongea na wanajumuia wa Ghuba hio, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Misitu,  Saidi Juma Ali, amesema jamii inatambua umuhimu wa uwepo bahari ndani ya viswa vya Zanzbar, lakini bado kumekua na ongezeko la uharibifu, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Alieleza baadhi ya faida za utunzaji wa Koko ni pamoja na kuhifadhi fukwe, kuhifadhi mazalia ya samaki na kupata uvuvi wenye faida,  kwani hazipo kwa ajili ya kijiji pekee bali ni kwa taifa zima.

Amesema, bado ipo haja ya kulinda koko na Serikali ipo tayari kupambana na wale wote watakao kiuka, hivyo ni vyema  Kamati ziwe  tayari kutoa mashirikiano,  ili kupata ubora katika suala la maendeleo.

Amesema serikali inategemea kupata taarifa za awali kutoka kwa wanajumuia na wanakamati wa hifadhi na kuacha kufanya muhali kwa waharibifu, kwani halitafikiwa lengo lililokusudiwa.

‘‘Ukweli Uwazi na Uaminifu ndio nyenzo pekee katika ufanisi na utekelezaji wa majukumu ya kazi na si vyenginevyo’’alisema