GENEVA, USWISS
MKUU wa Shirika la Fedha Duniani IMF Kristalina Georgieva, ameyatolea wito mataifa tajiri duniani kutoa misaada zaidi kwa mataifa maskini ili yaweze kuhimili athari za janga la corona na uharibifu wa kiuchumi unaotokana na janga hilo.
Akionya juu ya tofauti inayoongezeka kati ya mataifa tajiri na maskini, Georgieva amelitolea wito kundi la nchi 20 zilizostawi zaidi kiuchumi duniani G20, kuchukua hatua kuzilinda nchi zinazoendelea kutokana na kubaki nyuma katika upatikanaji wa chanjo na ufadhili ili kuufufua uchumi wao.
Katika ujumbo wa blogi kuelekea mkutano wa wiki hii wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka mataifa ya G20, mkuu huyo wa IMF amesema mataifa maskini yanakabiliwa na pigo mara mbili na kuishiwa na mbio dhidi ya virusi vya corona, jambo ambalo limepelekea kushindwa katika uwekezaji hivyo kuzisaidia nchi hizo kutazisaidia kuweka msingi wa ukuaji wa uchumi.