TOKYO, JAPANI

MAMLAKA za afya kote nchini Japani zimethibitisha visa vipya zaidi ya 9,500 vya virusi vya korona kwa mara ya kwanza tangu janga hilo lilipoanza.Tokyo bado ni kitovu cha maambukizi hayo ambapo maofisa  walitangaza zaidi ya visa 3,000 kuwahi kutokea kwa siku.

Hatua za dharura za Japani si kali kama kufunga nchi kunakotekelezwa katika nchi nyengine.

Maofisa wa Japani wanaweza kuwarai  wakaazi kuepuka matembezi yasiyo ya lazima na kuitaka mikahawa na baa kufunga mapema.Hali ya dharura ilichochea uamuzi usio wa kawaida wa kufanya karibu mashindano yote ya Olimpiki bila watazamaji.