MAPUTO, MSUMBIJI

MAOFISA wa usalama nchini Msumbiji wamesema kikosi cha jeshi la Rwanda vilivyotumwa kwenda Msumbiji kusaidia kupambana dhidi ya  waasi vimewauwa wanajihadi wasiopungua 30.

Maofisa hao wameeleza kuwa wanajeshi walikuwa wakifanya doria katika msitu uliopo karibu na mji wa bandari wa kaskazini wa Palma huko ndipo walipokutana na wanamgambo hao.

Inaelezwa kuwa takriban ya wanajeshi 1,000 wa Rwanda walitumwa Msumbiji mapema mwezi huu.

Aidha Jumuiya ya kusini mwa Afrika pia inapeleka wanajeshi na vikosi vya Ureno vinasaidia kufundisha jeshi la Msumbiji.

Takriban ya watu 800,000 wamehama makazi yao kutokana na uasi uliokithiri katika maeneo hayo kwa miaka minne, huku maelfu ya watu wakiuawa.