NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIPA wa kikosi cha Dodoma Jiji inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara,Aron karambo ,amemwaga wino kukitumikia kikosi cha Tanzania Prisons.

Karambo aliwahi kuwatumikia Tanzania Prisons kwa misimu mitano mfululizo kabla ya kutua Dodoma Jiji.Akizungumza na Zanzibar Leo , Karambo alikiri kurudi Tanzania Prisons, ili kutafuta changamoto nyingine.

Alisema ameitumikia Dodoma jiji na imetosha hivyo mabosi wake hao wa zamani walipo mfuata hakuona sababu za kuwakataa.Karambo aliongeza  atacheza timu hiyo mpaka pale atakapo ona inatosha ataondoka nakwenda sehemu nyingine, ambayo itamuhitaji kwani yeye ni mchezaji hivyo timu yoyote itakayomuhitaji hatokua na hiyana kama kuna uhakika wa nafasi.

“Nilikuwa napata nafasi Dodoma lakini nimeamua kusaini Prisons ili kubadilisha changamoto, sijaona ubaya wowote kurudi nilipotoka ikiwa wao ndio walio hitaji huduma yangu,”alisema