PROFESA wa skuli ya biashara ya Chuo cha Stanford nchini Uingereza aliwahi kusema kuwa kazi unayofanya inasababisha kukatisha uhai wako taratibu, lakini watu wengi hawaji kuhusu hilo

Katika kitabu chake alichokichapisha hivi karibuni alichokiita ‘kufa kwa ajili ya mshahara’, Prof. Pfeffer alisema kazi unayofanya na mifumo yake taratibu inatafuna uhai wako

Katika kitabu hicho anazungumzia tuko la Kenji Hamada, mwenye miaka 42 aliyekufa kwa mshtuko wa moyo akiwa kwenye dawati lake kazini jijini Tokyo. Nilifanya kazi saa 72 kwa wiki na ilikua inanichukua saa mbili kufika kazini.

Kabla ya kifo chake, alifanya kazi siku 40 mfululizo bila kupumzika na mjane wake anasema Kenji alikuwa na msongo mkubwa wa mawazo.

Huo ni moja kati ya mifano iliyokuwa kwenye chapisho lake, ambapo anaeleza madhara ya mfumo wa kazi ambao wakati mwingine ‘si ya kibinaadamu’ kutokana na majukumu makubwa ya kazi.

Kwa mujibu wa ushahidi Prof. Pfeffer, nchini Marekani asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waumwe na asilimia 7 wanasema walilazwa hospitali kutokana na sababu zinazohusiana na kazi.

Makadirio yake ni kwamba msongo una uhusiano na vifo vya wafanyakazi 120,000 wa Marekani. Kwa mtazamo wa kiuchumi, msongo umewagharimu waajiri zaidi ya dola za Marekani 300,000 kwa mwaka nchini Marekani.

Kazi sasa zimekua si za kibinaadamu. Kwa upande mwingine, makampuni yameacha kuwajibika kwa ajili ya wafanyakazi wao. Lakini changamoto za kiuchumi zimeongezeka, hofu ya kukosa ajira pia inaongezeka.

Katika benki za uwekezaji, kwa mfano, kuna namna ya ufanyaji kazi, unakwenda nyumbani kwako kuoga na kurejea ofisini. Katika mfumo huo, waajiriwa wengi huingia katika uraibu wa madawa, kwa sababu wanaishia kutumia Cocaine na madawa mengine ili wawe macho.

Mfanyakazi wa kiwanda, rubani wa ndege, mwendesha lori, wana idadi ya saa za kufanya kazi. Lakini kuna kazi nyingine hakuna saa maalumu za kazi.

Lakini nani anawajibika kwa vifo hivi? Waajiri na serikali zinawajibika kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu suala hili. Ni kazi kubwa tunapaswa kufanya kitu kwa ajili ya kukomesha hili. Lakini hatutaweza kufanya chochote kama mtu mmoja mmoja.

Kama unataka kutatua tatizo yapaswa kuwa katika utaratibu ambao utatoka kwa mtindo wa sheria. Mazingira mabaya ya kazi husababisha maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu.

Lakini tukizungumzia gharama, makampuni yanaweza kuleta hoja kuwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa kazi kutaathiri kipato cha kampuni.

“Tunajua kuwa watu walio katika msongo wa mawazo wako katika nafasi kubwa ya kuacha kazi”.Tunajua kuwa wafanyakazi wasio sawa kisaikolojia hawawezi kuizalishia kampuni inavyopaswa”, Profesa Pfeffer.

Alitolea mfano kuwa inafahamika kuwa Marekani na Uingereza zaidi ya 50% ya siku za kazi hupotea kwa sababu ya wafanyakazi kutokuwepo kutokana na msongo wa kazi.

Hivyo kuna athari kubwa kwa mfanyakazi mgonjwa anayekwenda kazini na asifanye kazi kama anavyotakiwa. Hali hii hui