LONDON, UINGEREZA

JESHI la polisi mjini London limesema kijana wa kiume mwenye miaka 15 ambaye wazazi wake ni Warundi ni mmoja wa watoto wawili waliokufa baada ya kuchomwa visu Jumatatu kusini mwa jiji la London.

Habimana mwenye umri wa 15, alichomwa kisu katika eneo la Woolwich New Road, Woolwich kusini mwa London saa 11: 25jioni ambapo polisi waliukuta  mwili wake chini na pembeni yake kulikuwa na visu vitatu.

Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kusaidia kuokoa maisha yake lakini juhudi zao hazikufanikiwa, na kwamujibu wa ripoti ya polisi alifariki.

Hata hivyo kijana mwingine wa miaka 15 tayari ameshakamatwa kwa shutuma za kumuua Habimana.

Kwamujibu wa taarifa zagazeti la Uingereza ‘The Standar’, imesema kuwa rafiki wa Habimana wamesema alikuwa na ndoto ya kuwa wakili baada ya kumaliza masomo.

Jumatatu iliyopita , Keane Flynn-Harling mvulana wamiaka 16 pia aliuliwa kusini mwa London, ambapo mwanaume mwenye umri wa miaka 29 alikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo chake.

Inaelezwa kuwa eneo la Woolwich mjini London linalokaliwa na watu wengi wa asili ya Afrika na Carribean ni eneo linalokabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya ghasia na wizi wa kutumia silaha.