KAMPALA, UGANDA

WIZARA ya Afya nchini Uganda imefunga kituo cha kibinafsi cha afya, Selmek Medical Services Ltd, kutoa huduma za upimaji wa Covid-19 kutokana na udanganyifu wa matokeo.

Barua ya Julai 21 iliyotolea  na Dk Henry Mwebesa,Mkurugenzi Mkuu wa huduma za afya katika wizara hiyo ilionyesha kuwa kituo hicho hakijapewa idhini na serikali kufanya vipimo vya  Covid-19.

Wizara ya Afya, kupitia ripoti kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe na matokeo mengine ya maabara, imeona kiwango cha juu cha matokeo ya udanganyifu ya Covid-19 kwa sampuli zinazohusiana na kituo hicho.

Akijibu barua iliyotolewa, Eric Mivule, mkuu wa Huduma za Matibabu za kituo hicho, alisema hawezi kulaumiwa kwa sababu hafanyi upimaji wa Covid-19.

“Sijapima Covid-19, ninachokifanya ni kukusanya sampuli na kuzipeleka Chuo Kikuu cha Makerere,wanatutumia matokeo na sisi tunapeleka matokeo kwa wateja”.

Mkuu wa maabara ya upimaji wa Chuo Kikuu cha Makerere Covid-19, Prof Moses Joloba, alisema ikiwa maabara ya upimaji wa Chuo Kikuu ina matatizo Wizara ya Afya ingeliifunga .

Kusimamishwa kwa kituo hicho kunatokana na Serikali kukabiliwa na ripoti zilizoenea za wasafiri wanaotoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, ambao walikuwa na vyeti hasi vya Covid-19, lakini baadaye wakapata virusi vya ukimwi katika nchi walizoelekea.